Home Uncategorized SIMBA YAENDELEA KUTOA TAHADHARI NA SOMO KWA MASHABIKI KUHUSU CORONA

SIMBA YAENDELEA KUTOA TAHADHARI NA SOMO KWA MASHABIKI KUHUSU CORONA


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ni muhimu kwa mashabiki kuzingatia kanuni na muongozo uliotolewa na Serikali wakati ligi itakapoendelea pale ilipoishia.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 kwa msimu wa 2019/20.

“Kikubwa ni kuendelea kuchukua tahadhari wakati wa mechi za ligi pamoja na nyingine ambazo zinaendelea, kikubwa ni kuzingatia kanuni na taratibu ambazo zimetolewa na Serikali kupitia Wizara ya afya.

“Mashabiki ni muhimu kuzingatia kuvaa barakoa wakati wa kuingia uwanjani, kunawa kwa maji tiririka bila kusahau umbali wa mita moja kati ya shabiki na shabiki, Corona ipo na lazima tuendelee kuchukua tahadhari,” amesema.

SOMA NA HII  WAWILI WANAOWINDWA NA SIMBA KUTIMKIA MOROCCO