Home Uncategorized ALIYEWAUA SIMBA TAIFA YUPO TAYARI KUWAVAA KWA MARA NYINGINE, ATOA AHADI KUBWA

ALIYEWAUA SIMBA TAIFA YUPO TAYARI KUWAVAA KWA MARA NYINGINE, ATOA AHADI KUBWA


BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Julai 12, Uwanja wa Taifa.

Morrison alikuwa kwenye mvutano na Yanga kutokana na ishu ya mkataba ambapo kwa sasa inaelezwa kuwa tayari kila kitu kimekamilika kwa mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki kurejea uwanjani.

Alirejea mazoezini Julai 2 akiwa ni mwenye furaha na hajasafiri na timu iliyokwenda Mara ambapo kesho itakuwa na mchezo dhidi ya Biashara United.

Morrison amesema:”Nipo na furaha kurejea ndani ya Yanga na mimi ni mchezaji wa Yanga hivyo nitafanya kazi yangu kwa kuwa ninapenda kucheza kwa furaha.

“Kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba nipo tayari na nikipata nafasi ya kufunga nitafunga kwani kazi ya mchezaji ni kutimiza majukumu yake,” amesema.

Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hatamtumia kwenye mchezo wa Biashara United ila Morrison amemwambia yupo tayari kucheza.

“Masuala yake mengine mimi siwezi kuzungumzia ni juu ya uongozi ila mchezaji ameniambia yupo tayari kucheza kwa ajili ya timu na kwenye mchezo wetu dhidi ya Biashara United sitamtumia,” amesema. 

Morrison alifunga kwenye mchezo wake wa kwanza wa dabi mbele ya Simba Uwanja wa Taifa Machi 8 wakati Yanga ikishinda bao 1-0.

SOMA NA HII  WACHEKA NA NYAVU NDANI YA LIGI KUU ENGLAND HAWA HAPA