Home Uncategorized VITA YA KUSHUKA DARAJA BADO MBICHI

VITA YA KUSHUKA DARAJA BADO MBICHI


 VITA ya kushuka daraja ni kama imezidi kuwa mbichi kutokana na timu kugongana pointi huku zikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Ni Singida United pekee yenye uhakika wa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kujikusanyia pointi 18 ikiwa imecheza mechi 37.

Ugumu upo kwa hawa jamaa na pointi zao ili kujua nani ni nani lazima zicheze na mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa Julai 26, :-Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila ipo nafasi ya 15 kibindoni ina pointi 42.

Mbeya City iliyo chini ya Amri Said ipo nafasi ya 16 ina pointi 42.

Mbao FC ipo chini ya Felix Minziro ipo nafasi ya 17 ina pointi 42.

Alliance FC inamaliza utata ikiwa nafasi ya 18 na pointi 42 zote zimecheza mechi 37.

Nani ni nani Kwenye kushuka ama kucheza playoff ni Julai 26 baada ya dk 90.

SOMA NA HII  YANGA YAIPIGA KIJEMBE KIMTINDO SIMBA ISHU YA CHAMA