Home Uncategorized MANCHESTER UNITED YAINGIA ANGA ZA BARCELONA

MANCHESTER UNITED YAINGIA ANGA ZA BARCELONA


MANCHESTER United ipo tayari kulipa pauni milioni 153 kupata saini ya nyota kinda wa Barcelona, Ansu Fati ili ajiunge na kikosi hicho.

Ripoti zinaeleza kuwa winga huyo mwenye miaka 17 atakuwa mbadala wa nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ambaye dau lake linatajwa kuwa pauni milioni 108.

Fati amecheza jumla ya mechi 33 kwenye mashindano yote ndani ya Barcelona msimu uliopita na alitupia jumla ya mabao nane. United inahitaji saini yake kwa kuwa bado ni kinda wanaamini atakuwa na faida kubwa akitua ndani ya kikosi hicho.

Barcelona bado haijafikiria kumuacha kinda huyo kwa kuwa amekuwa akipata malezi akiwa chini ya staa wa timu hiyo, Lionel Messi ambaye inaelezwa kuwa anahitaji kuondoka ndani ya timu ya Barcelona.

Sancho ambaye ni winga pia msimu uliopita alihusika kwenye jumla ya mabao 40 ambapo alifunga mabao 20 na kutoa jumla ya pasi 20.

SOMA NA HII  UNITED BADO HAWAJAMPOTEZEA SANCHO