Home Uncategorized MECHI YA UFUNGUZI WA LIGI KUU BARA KUPIGWA AGOSTI 30

MECHI YA UFUNGUZI WA LIGI KUU BARA KUPIGWA AGOSTI 30

 


MABINGWA wa Ligi Kuu Bara Simba kwa msimu wa 2019/20 wanatarajiwa kukutana na washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho, Namungo FC, Agosti 30, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Mchezo huo utakuwa ni wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6.

Namungo itakuwa na hasira za kufungwa mabao 2-1 mbele ya Simba kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Nelson Mandela huku Simba ikiwa na hesabu za kuanza kukusanya mataji mapema kabisa kabla ya ligi kuanza kuchanganya.
SOMA NA HII  WATATU WA KIKOSI CHA KWANZA KUBAKI BONGO SIMBA IKIKWEA PIPA KUWAFUATA UD SONGO