Home Uncategorized WATATU WA KIKOSI CHA KWANZA KUBAKI BONGO SIMBA IKIKWEA PIPA KUWAFUATA UD...

WATATU WA KIKOSI CHA KWANZA KUBAKI BONGO SIMBA IKIKWEA PIPA KUWAFUATA UD SONGO


IMEELEZWA kuwa nyota watatu wa kikosi cha kwanza wa timu ya Simba watabaki Bongo wakati timu ikikwea pipa kuelekea nchini Msumbiji kuivaa UD Songo.

Simba inatarajia kukwea pipa kesho kuifuata UD Songo kwenye mchezo wa awali wa kimataifa wa Ligi ya Mabigwa kabla ya kurudiana na mabingwa hao wa Msumbiji baada ya wiki mbili, Dar.

Wachezaji hao ni pamoja na kipa Aishi Manula, kiungo Ibrahim Ajibu na mshambuliaji Wilker raia wa Brazil.

Sababu kubwa inaelezwa ni pamoja na kusumbuliwa na majeraha kwa wachezaji hao pamoja na sababu nyingine za kiufundi.

SOMA NA HII  LIVERPOOL INA NAFASI YA KUTWAA TAJI LA ENGLAND, KUNA MPANGO WA KUPUNGUZA DAKIKA 90