Home Uncategorized SIMBA QUEENS 5-0 BAOBAB QUEENS, YAIVUA UBINGWA JKT QUEENS

SIMBA QUEENS 5-0 BAOBAB QUEENS, YAIVUA UBINGWA JKT QUEENS

TIMU ya Simba Queens leo Agosti 5 imeibuka na ushindi wa mabao 5 -0 mbele ya  Baobab Queens kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Mabao ya Simba yalifungwa na Mwanahamisi Omary aliyetupia mawili,Opah Clement alitupia bao moja, sawa na Dotto Evarist  huku kipa Zubeda Mgunda akitupia bao moja kwa mkwaju wa penalti.

Ushindi wa leo unaifanya Simba Queens kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi ya Wanawake kwa kuwa wamefikisha jumla ya pointi 53 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote kwa sasa ndani ya ligi hiyo.

Imebakiwa na mechi mbili za kucheza ambazo ni dhidi ya Alliance Girls  na TSC Queens yote hiyo itakuwa kanda ya ziwa Ushindi huo unaifanya kuivua JKT Queens ubingwa jumlajumla kwa kuwa msimu uliopita ilitwaa taji hilo.

SOMA NA HII  HAWA HAPA 11 WANATAJWA KUVAA JEZI YA SIMBA MSIMU UJAO