Home Uncategorized NINJA AFICHUA UDHAIFU WA KAGERE, MUGALU

NINJA AFICHUA UDHAIFU WA KAGERE, MUGALU

 



BEKI wa kati wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amefunguka kuwa, ni kazi rahisi kuwadhibiti washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na Chris Mugalu kama tu utafuata kanuni za ulinzi na kutocheza na presha.

Ninja alifanikiwa kuwazuia Kagere na Mugalu kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi Jumatano iliyopita uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ubingwa baada ya ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 ambapo Simba haikupiga shuti lolote lililolenga lango.

Akizungumzia siri ya kuwazuia Kagere na Mugalu, Ninja amesema: “Nadhani jambo kubwa unapocheza kwenye safu ya ulinzi ni kuhakikisha unacheza kwa nidhamu na kufuata maelekezo ya walimu, na kuachana na tabia ya kucheza kwa presha.

“Siyo mara ya kwanza kwangu kucheza na dhidi ya Kagere hivyo namjua vizuri kwa kuwa nimewahi kucheza dhidi yake na najua kama unacheza kwa umakini na kutompa nafasi basi hawezi kuwa na madhara,”

SOMA NA HII  AZAM FC: TUPO TAYARI KUWA WA KIMATAIFA