Home epl LONDON DABI LEO, TOTTENHAM YAIPIGA MKWARA ARSENAL

LONDON DABI LEO, TOTTENHAM YAIPIGA MKWARA ARSENAL

 JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Tottenham Hotspur amesema kuwa haangalii chini bali anaangalia juu kwa kuwa wapinzani wake leo Arsenal amewaacha kwa tofauti ya pointi 7.

Leo Machi 14, Tottenham itakuwa Uwanja wa Emirates kusaka pointi tatu mbele ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:30 usiku na unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa timu hizo.

Hii ya leo ni London Dabi na mchezo wa kwanza Tottenham ilishinda mabao 2-0 hivyo leo Mikel Arteta vijana wake wana kazi ya kulipa kisasi.

Mourinho amesema :”Kwa sasa mimi siangalii chini ila ninaangalia juu ambapo wapo wapinzani wangu wakubwa, yule ambaye yupo chini hanipi presha kikubwa ni kuona vijana wanapambana na kupata pointi tatu,”. 

Arteta amesema kuwa wapo tayari na wanaamini watafanya vizuri kwenye mchezo wao mbele ya wapinzani wao.

“Tottenham ni bora kila eneo hilo lipo wazi ila halitupi presha, vijana nimewaambia kwamba wana kazi ya kufanya uwanjani kusaka ushindi,” .


SOMA NA HII  KOCHA MPYA CHELSEA AANZA KAZI NA 'GUNDU'...ADAI KUONA 'MAPICHA PICHA' KWA WACHEZAJI...😂😂😂...