Home Simba SC MUONEKANO MPYA WA AJIBU WAZUA GUMZO KINOMA

MUONEKANO MPYA WA AJIBU WAZUA GUMZO KINOMA


 WAKIWA nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22, ghafla gumzo kubwa limekuwa juu ya muonekano mpya wa kiungo wa Simba, Ibrahim Ajibu.

Nyota huyo ambaye hakuwa na wakati mzuri kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa alicheza jumla ya mechi 7 kati ya mechi 34 ambazo timu hiyo ilicheza na kutwaa taji la Ligi Kuu Bara kwa sasa amekuwa katika muonekano mpya.

Baada ya picha ya Ajibu kuchapishwa kupitia ukurasa wa Instagram wa Simba wadau wakaidaka juu na kuangusha maoni yao kwamba huyo ndiye mrithi wa Chama na wengine wakidai kwamba amekuwa kibonge huku wale kutoka nchini Brazil wakiisifia.

Mbali na wadau pia moja ya waliodondosha maoni ni pamoja na Gerson Fraga aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Simba katika nafasi ya kiungo mkabaji na alikuwa anitwa mkata umeme.

Mkata umeme huyo kutoka Brazil, alidondosha maoni yake kwenye picha hiyo kwa kusema, “Fundi”.

Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya msimu wa 2021/22 ambapo wachezaji baadhi ambao hawajaitwa timu zao za taifa wanaendelea na majukumu ya maandalizi ya msimu mpya.

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA SC WALA KIAPO KUMALIZIA KAZI YA DAR...HISTORIA KURUDIWA..?