Home Habari za Simba Leo MCHEZAJI WA ZAMANI SIMBA…AISHITAKI TIMU YAKE FIFA

MCHEZAJI WA ZAMANI SIMBA…AISHITAKI TIMU YAKE FIFA

Nicholas Gyan na Habari za Simba

Aliyekuwa Kingo wa zamamni wa Simba Raia wa Ghana Nicholas Gyan, anayeitumika Singida Fountaine Gate, ameifungulia madai, timu  hiyo kwenye Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA),akitaka uongozi wa Singida FG kumlipa deni analowadai ili mambo yasiwe mengi.

Gyan alirudishwa Singida baada ya FIFA, kuipa siku 45 timu hiyo kumlipa deni la ada ya usajili huku malimbikizo ya mishahara wakiwa wamefanikiwa kuyatatua.

Kwa mujibu wa Mwanaspoti, Gyan alisema anaidai timu hiyo Sh 50 Milioni ambazo ni malimbikizo ya usajili wa kujiunga na timu hiyo iliyokuwa ni Sh100 milioni walimpa nusu hadi sasa hawajamkamilishia.

“Ligi imeisha na mimi bado nipo Tanzania sijarudi nyumbani nasubiri fedha yangu niliongea na viongozi walikubali kunilipa lakini naona wananiambia niondoke watanilipa nikiwa kwetu,” alisema Gyan na kuongeza;

“Siwezi kuondoka bila hiyo fedha kwani mkataba wa hilo deni umeisha natakiwa kulipwa kiasi changu chote ili niweze kutafuta maisha mengine nje ya Singida Fountain Gate.”

Uongozi wa Juu ulipotafutwa kuzungumzia madai hayo ya mchezaji simu zao ziliita bila kupokelewa, lakini Afisa Habari wa Singida FG, Joseph Mkoko alisema migogoro yote kuhusu timu hiyo na wachezaji watatolea ufafanuzi hivi karibuni.

“Msimu ndio umeisha hivi karibuni mambo ni mengi yamepita hapo katikati viongozi wa juu watakaa na kufanyia kazi changamoto zote na muda ukifika ufafanuzi utatolewa kwa taarifa maalum ya timu,” alisema.

SOMA NA HII  MOLINGA: CHAMA HAPATI NAMBA YANGA...NI MUDA SAHIHI