Home Habari za Yanga Leo YANGA INALIPA MISHAHARA MIZURI…YATUMIA BIL 7 KUWALIPA…PACOMEE,AZIZ KI

YANGA INALIPA MISHAHARA MIZURI…YATUMIA BIL 7 KUWALIPA…PACOMEE,AZIZ KI

Habari za Yanga leo

KLABU ya Yanga inaonyesha kuwa soka kwa sasa ni ajira ndiyo maana kwenye matumizi yao, mishahara imechukua fedha nyingi zaidi kuliko kitu kingine chochote ambapo imekwenda karibia nusu ya bajeti yao baada ya kutumia Sh7 bilioni.

Hii inaonyesha kuwa ni usahihi kuwa mishahara ya Yanga ni mikubwa kama ambavyo imekuwa ikielezwa.

Ishu nyingine inayoonekana kuchuma fedha zaidi Yanga ni uhamisho wa wachezaji ambapo waliwahamisha kina Pacome Zouazoa na Joseph Guede pamoja na mastaa wengine kwa Sh3.5 bilioni likiwa ndiyo eneo lingine ambalo limeshika nafasi ya pili kwa matumizi ya fedha.

MASWALI AMBAYO WENGI WANAJIULIZA.

Yanga imetumia zaidi ya kile ambacho imekusanya, ikiwa ndiyo timu iliyofanikiwa zaidi kwenye soka hapa Tanzania kwa msimu uliopita.

Timu hiyo ilichukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la FA, lakini ilivuka lengo la mafanikio kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika zaidi kuliko wengine wote.

Hii ina maana kuwa Yanga ambayo ilipata Sh2.3 bilioni baada ya kufika robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kama ingemaliza kwenye tegeti yao ya hatua ya makundi basi ingekuwa na hasara ya zaidi kwa kuwa ingekusanya dola 700,000 ambazo ni Sh1.8 bilioni.

Swali ambalo wengi wanajiuliza ni kama Yanga ambayo imetwaa makombe yote msimu huu, ina wadhamini wengi zaidi, ina mashabiki kuliko timu nyingine tena wanaolipa kadi za uanachama ina hasara nani yupo salama kwenye soka nchini?

Inaonekana kuwa timu ambazo zinawania ubingwa na Yanga ambazo hazijachukua ubingwa wowote na hazina mashabiki wengi wanaoingia uwanjani na kulipa viingilio basi zina hasara kubwa zaidi.

Fedha nyingine:

Kipengele hiki kimeonekana kuwasumbua mashabiki wa soka nchini na kila mmoja aliyesikiliza ameshindwa kukielewa na kujiuliza ilikuwaje hakikuwekwa kwenye mchanganuo halisi?

Mchanganuo wa matumizi ya Yanga hauna shida unajieleza, lakini tatizo linaonekana kwenye eneo la mapato, Yanga inaonyesha haki ya matangazo iliingiza Sh10 bilioni, mapato ya mlangoni iliingiza Sh1.4 bilioni ada za uanachama ikaingiza Sh613.3 milioni zawadi za ushindi Sh3.4 bilioni.

Huku kote hawana shida wanauliza mapato mengine ya Sh5.4 bilioni ni fedha zilizotoka wapi na mbona ni nyingi?

Hili limekuwa swali kubwa kwa mashabiki ambao wanaamini kuwa kulikuwa na nafasi ya kuwaeleza mashabiki fedha hizo zimetoka wapi.

Lakini wengi wanafikiri pia walikuwa wanatakiwa kufahamu mauzo ya jezi yameingiza shilingi ngapi ili msimu ujao wanunue zaidi kipengele ambacho hakipo kwenye jedwali, labda ndiyo mapato mengine?

SOMA NA HII  MAPYA YAIBUKA...SAKATA LA AZIZI K YANGA..HERSI AFUNGUKA