Home Habari za Simba Leo SIMBA YAMBADILISHIA MAJUKUMU CALVIN MAVUNGA

SIMBA YAMBADILISHIA MAJUKUMU CALVIN MAVUNGA

HABARI ZA SIMBA-CALVIN MAVUNGA

BAADA YA SIMBA kufanya sajili za maana kwa msimu huu, wakileta maingizo mapya ya kutosha na benchi jipya la ufundi chini ya kocha Fadlu Davids.

Simba imeendelea kwa kufanya maboresho zaidi haswa kwa benchi la ufundi, na eneo lililofikiwa ni kwa mtathimini wa michezo Calvin Mavunga.

Mabosi wa Simba, wameamua kumbadilishia majukumu aliyekuwa mtathimini viwango vya wachezaji (perfomance analyst), Culvin Mavunga, raia wa Zimbabwe na sasa atakuwa GPS Tracking.

Kazi ya Mavunga itakuwa ni kufuatilia mienendo ya wachezaji uwajibikaji wao uwanjani kwa kutumia vifaa maalum, ikiwemo mikimbio na nguvu iliotumika, kujua utimamu wao wa mwili.

Mabadiliko hayo, yamefanywa baada ya Simba, kumuajiri mtathimini mpya wa viwango vya wachezaji uwanjani ambaye ni raia wa Afrika Kusini, Mueez Kajee. Taarifa za ndani zinasema; “Tumeamua kuboresha maeneo mbalimbali likiwemo la Mavunga kumpa majukumu mapya yenye afya kwa klabu yetu.”

Kiongozi huyo, alisema wanaheshimu kazi kubwa iliyofanywa na Mavunga, ambayo iliwasaidia kufahamu mbinu na udhaifu wa timu pinzani, ndio maana wameona umuhimu wa kuendelea naye, ili kusaidia eneo lingine. Kabla ya Kajee, kujiunga Simba alifanya kazi hiyo na klabu ya Raja Club Athletic, Maritzburg United FC na Free State Stars ya nchini kwao Afrika Kusini.

Wachezaji wapya wa kigeni wa Simba ni mabeki, Steve Dese Mukwala M9, Joshua Mutale, Valentin Nouma na Chamou Karabou, viungo Debora Mavambo, Augustine Okejepha na Charles Ahoua wanaoungana na Fabrice Ngoma, Ayoub Lakred, Che Fondoh Malone, Freddy Michael na Willy Onana.

SOMA NA HII  KIZAAZAA CHA MZAMIRU YASIN KWENYE DABI, ROBERTINHO ALISEMA HIVI