Debora Fernandes Mavambo unaweza kusema amekabidhiwa mikoba mizito kutokana na uzi atakaotumia kuwa na namba iliyoacha rekodi ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids.
Debora Fernandes Mavambo kwa sasa pale Simba anavaa jezi namba 17, ambayo ilikuwa inavaliwa na Mwamba wa Lusaka Clatous Chama.
Kwa sasa Chama ameondoka Simba na kujiunga na watani zao Yanga, lakini akiwa huko Yanga ameendelea pia kuivaa jezi namba 17.
Tangu awe Simba Chama alifanya mambo makubwa sana akiwa na jezi hiyo mgongoni mwake, kwa misimu mitano aliisaidia timu hiyo kutwaa mataji mengi
Ikiwemo Ubingwa wa Ligi Kuu mara 4, ubingwa wa FA mara 2, na Ubingwa wa Mapinduzi mara 2, Ngao ya Jamii mara 2, Kuifikisha Simba hatua ya robo fainali Klabu Bingwa mara 4 na Kombe la Shirikisho mara 1.
Mavambo Fernandes licha ya presha kubwa ju ya jezi hiyo, lakini alijitambulisha vyema kabisa katika mechi ya kwanza ya Simba Day,akifunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-0.
Mavambo Fernandes alipiga shuti kali nje ya 18 na kufunga, huku aina yake ya uchezaji ukiwavutia wapenzi na mashabiki wa Mnyama.
Ni mchezaji ambaye anamuda kucheza namba Zaidi ya 1, anacheza kama kiungo wa chini, kiungo mshambuliaji na kiungo mchezeshaji.
Swali ni Kwamba ataweza kuitendea haki jezi namba 17? Muda utaongea Zaidi.