Home Habari za Simba Leo AHOUA AANZA KAZI SIMBA…MTAFURAHI NA SHOW

AHOUA AANZA KAZI SIMBA…MTAFURAHI NA SHOW

Habari za Simba- Ahoua

BAADA ya kuonesha makali na moto wake kwenye mchezo wa pili wa Ligi kuu ya NBC, Jean Charles Ahoua alifunga goli moja na kuhusika kwenye mabao mengine matatu ya Simba, hivyo aliweza kuhusika kwenye mabao yote manne ya dhidi ya Fountain Gate FC.

Mchambuzi wa michezo Hans Raphael amemuelezea mchezaji huyo, namna uwezo wake ulivyo.

“This young man was born to play football, alihitaji muda mchache kuisoma ligi ya Tanzania na kuanza kuwanyanyasa wapinzani.”

“Mguu wake wa kulia uliumbwa ku-assist,siyo kwa bahati mbaya msimu uliopita alitoa assist 12 kwenye ligi ya Ivory Coast…..kijana anajua muda sahihi wa kuachia  pasi kwa washambuliaji wake.”

“Leo ametoa assist (2) na goli (1) pia tukumbuke amepre-assist goli la Mukwala….ni wazi kwenye mechi mbili Ahoua ana assist (3) na goli moja,pia Kwenye hizo mechi mbili Simba wamefunga goli (7) na Ahoua kahusika kwenye goli (4) absolutely sensational”

“Ahoua alihitaji mechi chache kuisoma ligi ya Tanzania,na tayari amejua timu nyingi zinafinya nafasi kati kati ya uwanja hivyo yeye kama namba 10 ameamua kufanya mikimbio mingi ya uongo (Decoy movements) pembezoni mwa uwanja….na huko anafanya vitu vingi vitokeee”

“Hii haitoishia kwa Fountain Gate,bali timu nyingi zitaonja joto la Jini Charles Ahoua.”

“NB:Tujifunze kuwapa muda wachezaji.” Alimaliza kwa kusema hivi.

SOMA NA HII  MANARA AFUNGUKA KUHUSU MO DEWJI NA AINA YA WATU ANAOWAPENDA