Home Habari za Simba Leo AHMED ALLY AMJIA JUU ALI KAMWE…ACHENI KULALAMIKA

AHMED ALLY AMJIA JUU ALI KAMWE…ACHENI KULALAMIKA

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba Ahmed Ally ameshangazwa na kauli ya Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe, kuhusu mafanikio ya Simba kwa msimu huu.

Jana Simba na Yanga zilicheza michezo yao ya Ligi na zote zilifanikiwa kupata ushindi, sio tu ushindi bali ni ushindi wa bao moja tu kwa kila timu.

Ali Kamwe alitoa povu kwa Azam Media kuhusu caption zao za mechi, za Jana kuhusu matokeo ya mwisho.

Kwenye Caption ya Yanga iliandikwa “Kimoko” huku ya Simba ikiandikwa “Pointi tatu kwa Mnyama”

Ahmed Ally ametupia kijembe kingine kwenda kwa watani zao Yanga, kuwa Ubaya Ubwela unakwenda kuwafanya walalamikie kila mtu.

“Malalamiko yameanza mapema sana

mwaka huu na kila mtu atalalamikiwa kuanzia waandishi mpaka marefa na sisi imetuogopesha mbona wameanza mapema sana kulalamika” Ahmed Ally.

“Mpaka sasa waliolalamikiwa kwa Simba kufanya vizuri ni Waamuzi, Waandishi, Wachambuzi na AZAM TV.

“Kimsingi huko ni kutafuta kichaka ukweli ni kwamba wamepagawa na ubora wa Simba, na wametishika na kasi ya Mnyamaa

Sasa niwatangazie tuu sisi bado hatujaanza kutekeleza Ubaya Ubwela ule wenyewe wenyewe tukianza ndio mtajua ukifa hurudi”

Aidha Ahmed Ally amezungumza kuwa timu ya Yanga sio mbaya ila shida ni matarajio yanakwenda siyo .

SOMA NA HII  RASMII...INONGA ATUPWA SOKONI....AL AHLY, FAR RABAT ZAITWA MEZANI ...