Home Habari za Simba Leo BEKI WA ZAMANI SIMBA…ATUA BAROKA YA AFRIKA KUSINI

BEKI WA ZAMANI SIMBA…ATUA BAROKA YA AFRIKA KUSINI

HABARI ZA SIMBA-ABDI BANDA

ALIYEWAHI kuwa beki wa Simba SC na Coastal Union Abdi Banda amerejea katika kikosi cha Baroka cha Afrika Kusini alichokitumikia akitokea Richards Bay.

Nyota huyo mara ya kwanza alijiunga na Baroka akitokea Simba Julai 12, 2017 na sasa amerejea tena baada ya awali dili lake la kujiunga na Singida Black Stars ya Ligi Kuu Bara iliyokuwa inamtaka kugonga mwamba mwanzoni mwa msimu huu.

Banda alisema alipata ofa kutoka klabu mbalimbali japo amefanya uamuzi sahihi kwa ajili ya maisha yake.

“Kama nilivyokwambia mwanzoni nilikuwa na ofa nyingi hadi falme za Uarabuni, ila nimeamua kurejea hapa kwa sababu kuna mambo ambayo tumekubaliana na nimefurahishwa nayo. Lengo ni kuendelea kupambana hiyo ndiyo kazi yangu,” alisema.

Banda aliyezichezea pia timu za Coastal Union, Mtibwa Sugar pamoja na Chippa United, Highlands Park na TS Galaxy za Afrika Kusini, amekuwa mhimili wakati akiitumikia Taifa Stars.

Nyota huyo amekuwa akisifika kutokana na uhodari wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani ikiwemo ya beki wa kati na kushoto kwa ufasaha, jambo ambalo limekuwa kivutio kwa makocha mbalimbali kumtumia kutokana na utulivu wake.

SOMA NA HII  HABARI ZA USAJILI SIMBA LEO...PACHA WA AZIZ KI NOUMA KUTUA UNYAMANI