Home Habari za usajili Simba leo HABARI ZA USAJILI SIMBA LEO…PACHA WA AZIZ KI NOUMA KUTUA UNYAMANI

HABARI ZA USAJILI SIMBA LEO…PACHA WA AZIZ KI NOUMA KUTUA UNYAMANI

HABARI ZA USAJILI SIMBA

HABARI za Usajili Simba zinaendelea kushika kasi kubwa,  ambapo taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinasema klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Burkina Faso na FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo, Valentin Nouma kwa ajili ya kuipata huduma yake.

Simba ambayo imepanga kujiimarisha zaidi kuelekea msimu ujao, inaamini kwamba beki huyo anayecheza kikosi cha Burkina Faso sambamba na kiungo wa Yanga Stephane Aziz Ki, anaweza kuwa mtu sahihi kwao.

Uamuzi wa Usajili wa Simba kusaka beki wa kushoto umekuja baada ya kumtumia kwa muda mrefu nahodha wao, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye anaonekana mpinzani wake ameshindwa kupatikana.

 Mbali na Nouma, Simba hapo awali ilikuwa ikitajwa kuwa kwenye mazungumzo na beki Joyce Lomalisa aliyemaliza mkataba ndani ya Yanga ambapo timu hiyo inaangalia uwezekano wa kumpata beki wa kushoto kwenda kusaidiana na Tshabalala.

Hadi sasa tayari Uongozi wa Simba umefanikiwa kunasa saini za wachezaji wazawa, ambapo mmoja wapo niLameck Lawi kutoka Coastal Union anayeweza kucheza nafasi mbalimbali kama beki wa pembeni, na beki wa kati.

Kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo ni suala  la muhimu kutokana na baadhi ya wachezaji wake kutumika kwa muda mrefu, ikiwemo Mohammed Hussein, Shomary Kapombe wote hawa wanahitaji watu wa maana wa kuwapa changamoto.

SOMA NA HII  FARID MUSSA AONGEZA MIWILI YANGA...KUMPA CHAMA JEZI NAMBA 17?