Home Habari za Simba Leo SHAFII DAUDA APINGA UREJEO WA MO DEWJI SIMBA

SHAFII DAUDA APINGA UREJEO WA MO DEWJI SIMBA

Habari za Simba- Mo dewji

BAADA ya Mohammed Dewji kutangaza kurudi Simba, na kuchukua nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi iliyoachwa wazi na Salim Abdallh ambaye Juni 11,  2024 alitangaza kujiuzulu, yameibuka mambo mengi, huku kila mtu aitoa maoni yake.

Moja kati  ya wadau wakubwa wa soka na mwandishi nguli wa michezo Shafii Dauda ametoa mtizamo wake, ambao umeonekana kupingwa na watu wengi haswa mashabiki wa Simba.

Dauda amepinga uwepo wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba,  kwa kusema Simba inatakiwa kuwa ya Mwenyekiti Mangungu.

“Mashabiki wa Simba waelewe hakuna mtu ambaye anapinga jitihada zilizofanywa na Mohammed Dewji , kila mtu anatambua mchango wake, Mjadala ambao tunajadili ni uhalali wa bodi ya Simba “

“Simba inatakiwa kuwa chini ya Mangungu lakini mashabiki hawataki kulisikia hilo , leo hii tunaambiwa Mo anarudi ! Je anakuja kuwa mwenyekiti wa bodi ipi ? “

“Ili bodi iwe hai ni lazima mchakato uwe umekamilika , huu mchakato wa Simba umekwama”

“Uongozi wa Simba uliopo ,upo kwa nguvu ya wanachama ambayo ndio Simba ya sasa hivi na kiongozi wao ni Mangungu na yeye ndio anayeendesha shughuli za kila siku za klabu”

Aidha ameongeza kwa kusema kwamba, Mohammed Dewji kama anataka kuongoza Simba, anatakiwa agombee na achaguliwe na wanachama kwenye uchaguzi mkuu.

“Mo kama anataka kuingia Simba na ili awe na nguvu kwa huu mfumo uliopo sasa hivi inabidi asubiri miaka minne ufanyike uchaguzi agombee kama Mangungu”

“Baada ya hapo atakuwa mwenyekiti wa Simba ambaye anatambulika kiutaratibu wa uendeshaji wa Klabu”

“Kinachofanyika sasa hivi ni kwa sababu Mo ana hela sana lakini lazima kuwe na utaratibu unaoeleweka na watu wasifiche vitu” Alisema Shafii Dauda.

Credit Clouds Fm.

SOMA NA HII  YANGA YAMRUDISHA MATOLA CHAP