BANDA:TUNAPIGA MATIZI KAMA KAWAIDA HUKU
ABDI Banda, beki wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars anayekipiga Highlands Park FC ya Afrika Kusini amesema kuwa bado wanapiga matizi kama kawaida na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona. Ligi Kuu ya Afrika Kusini imesimamishwa kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa.Banda amesema kuwa:-"Tupo tunachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona...
GUARDIOLA ANAWEZA KUSEPA NDANI YA MANCHESTER CITY, SABABU YATAJWA
EMANUEL Petit, mkongwe wa zamani wa timu ya Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa amesema kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Pep Guardiola anaweza kusepa ndani ya kikosi hicho.Nyota huyo amesema sababu itakayomfanya Guardiola kusepa ndani ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England ni kushindwa kujinasua kwenye sakata la kufungiwa na UEFA..City imefungiwa na UEFA kushiriki Ligi ya...
SARAKASI ZA USAJILI KWA BONGO HUWA NI PASUA KICHWA ANAYESEPA HUWA BORA
AMISS Tambwe ni nyota wa zamani wa Yanga na Simba alicheza ndani ya Ligi Kuu Bara kwa mafanikio makubwa na kuweza kushika chati ndani ya Yanga pia hata alipokuwa Simba.Emmanuel Okwi raia wa Uganda anayekipiga pia kwenye timu ya Taifa pia ni nyota wa zamani wa Simba na Yanga alicheza kwa mafanikio makubwa alipokuwa Bongo kwenye Ligi Kuu Bara. Wote...
MLINDA MLANGO YANGA: WASHAMBULIAJI WOTE BONGO WAPO VIZURI
MLINDA mlango namba mbili wa Yanga, Metacha Mnata amesema kuwa washambuliaji wote Bongo wapo vizuri ila kinachohitajika kwa mlinda mlango ni umakini.Akizungumza na Saleh Jembe, Mnata amesema kuwa kwenye kila mechi kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa alikuwa anakutana na ugumu kutoka kwa washambuliaji jambo ambalo lilikuwa linamfanya apambane kuwa bora."Kila mechi ina changamoto zake na ushindani wake ambao...
ISHU YA KAHATA, KAGERE NA SHIBOUB KURUDI BONGO SIMBA YAIACHIA SERIKALI
UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa unaiachia Serikali ishu ya wachezaji wao kurudi Bongo kutokana na wao kutokuwa na namna ya kufanya.Nyota wa Simba ambao ni Meddie Kagere, Francis Kahata na Sharaf Shiboub wapo nje ya nchi na mipaka kwao imefungwa kutokana na kujilinda na maambukizi ya Virusi vya Corona.Kagere yupo Rwanda, Kahata yupo Kenya na Shiboub yupo...
KAGERA SUGAR WAWAOMBA MASHABIKI KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA
MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa ni muhimu kwa wachezaji na mashabiki kuendelea kuchukua tahadhari juu ya Virusi vya Corona.Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa kila mmoja ni wajibu wake kuchukua tahadhari na kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona. "Kila mmoja ni wajibu wake kuchukua tahadhari na kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona kwani wakati uliopo...
ALIYEWATUNGUA SIMBA NA YANGA AJICHIMBIA BUNDA KWA SASA
SIXTUS Sabilo, mshambuliaji namba moja wa Polisi Tanzania amesema kuwa kwa sasa anaendelea kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona akiwa zake nyumbani Bunda.Akizungumza na Saleh Jembe, Sabilo amesema kuwa kwa sasa kuna mengi ambayo anayakosa kwenye mpira lakini hakuna namna ni lazima kujilinda kwanza kwani afya ni jambo la msingi."Kuna vitu vingi ambavyo tunavikosa kwa sasa lakini hamna namna...
MTIBWA SUGAR YAWATUMA WACHEZAJI KUWA MABALOZI KWA JAMII
UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa umewatuma wachezaji wao wa Mtibwa Sugar kuwa mabalozi kwenye jamii kuhusu janga la Virusi vya Corona.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema kuwa wamewambia wachezaji wao wawe makini na wahakikishe wanachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona."Tupo kwenye wakati mgumu kwa sasa ila imani yetu ni kwama hili...
SIMBA: YANGA WAISHUKURU GSM BILA WAO KUTUFUNGA INGEKUWA NDOTO
UONGOZI wa Simba umesema kuwa uongozi wa Yanga ni lazima waushukuru uwepo wa GSM ndani yao kwani isingekuwa hivyo hata kuwachapa kwenye mchezo wao uliochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa ingekuwa ni ndoto.Yanga iliibuka na ushindi huo kwa bao pekee lililofungwa na Bernard Morrison kwa mpira wa adhabu aliofunga akiwa nje ya 18 na kuwafanya Simba kuyeyusha pointi tatu...
YANGA WABISHI KWELI, WAIKOMALIA SIMBA KWA CHAMA
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umefikia hatua nzuri ya kuipata saini ya nyota wa Simba, Clatous Chama ili akacheze ndani ya Yanga msimu ujao.Chama amekuwa gumzo kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja jambo ambalo limewavutia Yanga ambao wanahitaji kuboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wamezungumza na meneja wa Chama...