Home Uncategorized TIMU YA SAMATTA YAAMBULIA KICHAPO TENA

TIMU YA SAMATTA YAAMBULIA KICHAPO TENA


ASTON Villa timu anayocheza nyota mtanzania, Mbwana Samatta jana imekubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Southampton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa St.Mary’s.

Aston Villa ina kumbukumbu ya kupoteza mechi mbili mfululizo ilianza mbele ya Spurs ya Jose Mourinho kwa kuchapwa mabao 2-1 na jana ilichapwa mabao 2-0.

Samatta ana kandarasi ya miaka minne na nusu ndani ya Aston Villa alijiunga akitokea KRC Genk ya Ubelgji ametupa bao moja ndani ya ligi hiyo na jana alishindwa kufurukuta.

Mabao ya wapinzani wao yalifungwa na Shane Long dakika ya nane na Stuart Armstrong alifunga bao la dakika ya 90 baada ya wachezaji wote wa Aston Villa kwenda kushambulia kona.

Aston Villa imebaki nafasi ya 17 ina pointi 25 imecheza mechi 27.

SOMA NA HII  ATLETICO MADRID, MANCHESTER UNITED ZAINGIA ANGA ZA BARCELONA