Home Uncategorized UONGOZI WA SIMBA WAHITAJI KUONGEZA MASHINE MBILI ZA KAZI, MAJINA YAO HAYA...

UONGOZI WA SIMBA WAHITAJI KUONGEZA MASHINE MBILI ZA KAZI, MAJINA YAO HAYA HAPA


UONGOZI wa Simba umesema kuwa mpango mkubwa kwenye kuboresha kikosi chao kwa sasa ni sehemu ya mshambuliaji ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.


Wakati Ligi Kuu Bara inasimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, safu ya ushambuliaji ya Simba ilikuwa inaongoza kwa kutupia mabao ambao ilikuwa imefunga mabao 63.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kuna ulazima wa kuongeza washambuliaji ili kuwa na mbadala pale ambapo mmoja akipata matatizo.

“Nilianza kukinoa kikosi nikiwa na mshambuliaji tegemezi mmoja ambaye yeye alikuwa fiti huku wengine wakiwa ni majeruhi, kwa sasa malengo yangu ni kuona kwamba kila nafasi inakuwa na mbadala wake jambo linalofanya nihitaji kuwa na washambuliaji zaidi.

“Hiyo itasaidia iwapo itatokea kutakuwa na wagonjwa ama tatizo lolote lile wao wataendelea kucheza bila hofu ila hawa waliopo pia wanafanya kazi kubwa,” amesema.

Miongoni mwa washambuliaji ambao wanatajwa kuwindwa na Simba ndani ya Bongo ni Relliants Lusajo anayekipiga ndani ya Namungo akiwa na mabao 11 pamoja na Paul Nonga anayekipiga Lipuli.
SOMA NA HII  KOCHA MKUU WA YANGA ATIA TIMU BONGO