Home Uncategorized MUANGOLA WA YANGA SAFARI YA KUSEPA IMEWADIA

MUANGOLA WA YANGA SAFARI YA KUSEPA IMEWADIA



CARLOS Carlinhos raia wa Angola mwenye uwezo wa kupiga mipira iliyokufa ndani ya kikosi cha Yanga huenda akatolewa kwa mkopo ama akaachwa Jumlajumla ndani ya kikosi hicho.

Habari zinaeleza kuwa kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ni sababu ya nyota huyo kuwekwa kando kwa kuwa ameshaondolewa kwenye mfumo.

Muangola huyo anasumbuliwa na majeraha ya nyonga ambayo aliyapata alipokuwa mazoezini jambo.

Hakuwa kwenye kikosi kilichoshinda mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji na hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Ihefu kesho,Desemba 23 Uwanja wa Sokoine.

Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga kuhusu suala hilo amesema kuwa kwa sasa wanajiendesha kidijidatal hivyo kila kitu kitawekwa kwenye mitandao yao.

Yanga ikiwa imetupia jumla ya mabao 25 amehusika kwenye mabao manne, amefunga mawili na ana pasi mbili za mabao.

SOMA NA HII  MITAMBO MIWILI YA KAZI YANGA NI BALAA, JEZI ZAO WOTE NAMBA SARE