Home Habari za Simba Leo SABABU ZILIZOMRUDISHA BANDA BAROKA

SABABU ZILIZOMRUDISHA BANDA BAROKA

HABARI ZA SIMBA-ABDI BANDA

WIKIENDI hii beki wa zamani wa Richard Bays, Abdi Banda alitambulishwa Baroka ya Afrika Kusini alikoondoka miaka sita iliyopita.

Banda kwa mara ya kwanza alijiunga na Baroka akitokea Simba Julai 12, 2017 na sasa amerejea tena baada ya kudai alikuwa akihitajika na timu kadhaa kutoka Uarabuni na Singida Black Stars.

“Nimerudi kupambana na kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri, mwanzoni nilikuwa na ofa nyingi hadi Falme za Uarabuni, ila nimeamua kurejea hapa kwa sababu kuna mambo ambayo tumekubaliana na nimefurahishwa nayo,” alisema Banda na aliongeza;

“Kwa hapa Afrika Kusini mimi ni mwenyeji, nimecheza timu mbalimbali, hivyo kurejea kwangu Baroka kutasaidia kuizoea kwa haraka ligi hiyo kwa sababu niliwahi kucheza muda kidogo.”

Kabla ya beki huyo kutumikia ligi hiyo aliwahi kuzichezea Coastal Union, Mtibwa Sugar pamoja na Chippa United, Highlands Park na TS Galaxy za Afrika Kusini na amekuwa mhimili wakati akiitumikia Taifa Stars.

SOMA NA HII  MIL 350 KUMSHUSHA PACHA WA PHIRI SIMBA SC....JAMAA LINAJUA HILOO...