Home Uncategorized ANTONIO CONTE AMPA MANENO YAKE ERIKSEN

ANTONIO CONTE AMPA MANENO YAKE ERIKSEN


ANTONIO Conte, Kocha Mkuu wa Inter Milan amesema kuwa nyota wake mpya, Christian Eriksen anahitaji muda ili kuzidi kuwa bora ndani ya kikosi hicho.

Eriksen nyota mpya wa Inter Milan aliyetoka Spurs, alifunga bao lake la kwanza mbele ya Ludogorets kwenye ushindi wa mabao 2-0 mchezo wa Kombe la Europa hatua ya 32.

Eriksen alifungua nyota yake dakika ya 71 na bao la pili la ushindi lilifungwa na Romelu Lukaku dakika ya 90+5 penalti.

“Amefanya vizuri kwenye mechi yetu tuliyocheza usiku Ila bado ana kazi ngumu ya kufanya ili kuwa bora zaidi.

“Nadhani ili awe imara ana kazi kubwa zaidi ya hapo, Ila tutamfanya awe bora na atafikia malengo aliyojiwekea nafasi yake ipo,” amesema.


SOMA NA HII  YANGA BABA LAO YAITUNGUA SIMBA YENYEWE YA KAGERE 1-0