Home Habari za Simba Leo AHMED ALLY ATAMBA NA USAJILI MPYA…JOSHUA MUTALE NI HATARI

AHMED ALLY ATAMBA NA USAJILI MPYA…JOSHUA MUTALE NI HATARI

Habari z Simba, Felix Sunzu Kuhusu Joshua Mutale

Simba imemtambulisha rasmi Joshua Mutale raia wa Zambia anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji kuwa mchezaji wao kwa miaka mitatu.

Kiungo huyo aliyekuwa akikipiga Power Dynamos msimu wa 2023/2024 amefunga mabao matano na asisti tatu kwenye mechi 26 alizocheza.

Joshua Mutale mwenye miaka 22 anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani tena kwa ufanisi kwani anaweza kucheza kama winga ya kulia, kushoto na wakati mwingine anacheza nyuma ya mshambuliaji yaani namba 10.

Akiwa Power Dynamos msimu uliopita, Joshua Mutale amefunga mabao matano na kuisaidia kupatikana kwa mengine matatu katika michezo 26.

Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo wa Kizambia alikutana na Simba kwa mara ya kwanza kwenye mechi za hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kule Zambia alikinukisha sana kwa kasi yake na akili kubwa ya kuficha mali.

Mechi ya Pili ilichezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar Es Salaam pia alisumbua sana mabeki wa Simba, kila upande aliokuwa akicheza alifanya balaa, kila mpira aliokuwa akiupata ulikuwa una madhara kwa wapinzani.

Ahmed Ally alipokuwa anauzungumzia usajili huu, alisikika akisema kwamba huyu ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na kasi.

“Tumemaliza kusajili kwa 97% muda wowote tunaanza kutambulisha, moja ya wachezaji tuliowasajili wanatoka DR Congo, Ivory Coast na Zambia, lakini kuna huyo mmoja anakimbia kama treni ya SGR” Ahmed Ally

Simba inaendelea na kutambulisha wachezaji wengine, na leo wametangaza kushusha chuma kingine ikiwa ni sehemu ya kutengeneza timu imara na tishio ndani ya Tanzania na Kimataifa.

Simba msimu uliomalizika aliishia nafasi ya tatu na kwenye mashindano ya kimataifa atacheza Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo wanahitaji kuweka heshima upande huo.

SOMA NA HII  CHAMA HAAMINI MACHO YAKE, UONGOZI WA SIMBA WAMFANYIA UMAFIA