SPURS WAMTAKA NYOTA WA JUVENTUS
PAULO Dyabala mshambuliaji wa Juventus amewekewa kwenye hesabu na klabu ya Totthenham ambayo inataka kuipata saini ya nyota huyo raia wa Argentina.Juventus ipo tayari kumuachia nyota huyo na inahitaji dau la pauni milioni 80 ili waongeze nguvu kwenye kikosi chao.Inaelezwa kuwa baada ya Juventus kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid nyota huyo alianza kuomba kusepa ndani ya kikosi hicho.
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la CHAMPIONI Jumamosi
KABLA LIGI KUU BARA HAIJAANZA, RATIBA YA LIGI KUU BARA KUFANYIWA MABADILIKO
WILFRED Kidao, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu ujao ikafanyiwa marekebisho.Kidao amesema kuwa mabadiliko hayo yanatokana na muingiliano wa mechi za kitaifa ambazo zitashirikisha timu nne msimu ujao."Haikuwa hesabu zetu kufanya hivi na hii inatokana na matarajio yetu ya timu ya Simba kuanza hatua ya...
NAHODHA MPYA WA YANGA HUYU HAPA, ARITHI KITAMBAA CHA AJIBU
PAPPY Tshishimbi, kiungo wa Yanga amekabidhiwa kitambaa cha unahodha ndani ya kikosi hicho kilichoweka kambi mkoani Morogoro.Kiungo huyo amekabidhiwa kitambaa hicho ambacho kilikuwa mikononi mwa Ibrahim Ajib ambaye amejiunga na Simba ambaye aliuchukua mikononi mwa Kelvin Yondani.Kambi ya Yanga imeanza Julai 7 na bado inaendelea na kambi hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao na michuano ya kimataifa.Mratibu...
MASHABIKI WAITWA UWANJA WA TAIFA AGOSTI 28 KUIPA SAPOTI TIMU YA TAIFA
CLIFORD Ndimbo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa ni wakati wa mashabiki kujitokeza kwa wingi Agosti 28 kuipa sapoti timu ya Taifa.Taifa Stars itamenyana na Kenya Agosti 28 uwanja wa Taifa mchezo wa kufuzu michuano ya Chan uwanja wa Taifa.Akizungumza na Saleh Jembe, Ndimbo amesema kuwa ni wakati wa Taifa kuungana kuipa sapoti timu ya...
YONDAN ANA BALAA, KAMBI YA SIMBA YAZIDI KUNOGA NI KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI
KESHO CHAMPIONI Jumamosi limesheheni habari kamili kuhusu kambi ya Yanga, Maandalizi ya Timu ya Taifa ya Tanzania bila kusahau kambi ya Simba
MATOLA: AKIPATIKANA MDHAMINI MKUU, MSIMU UJAO UTANOGA
SELEMAN Matola Kocha wa Polisi Tanzania amesema kuwa msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa endapo atapatikana mdhamini mkuu.Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa kwa sasa mambo bado hayajakaa sawa kutokana na kutopatikana mdhamini mkuu."Bado kwa sasa mambo hayajakaa sawa, endapo mdhamini mkuu atapatikana itasaidia kuleta ushindani na kila mmoja ataona namna ligi itakavyokuwa bora hivyo itapendeza kama mdhamnini...
ARSENAL WABISHI KINOMA WAKOMAA NA AUBAMEYANG
ARSENAL imesema kuwa haina mpango wa kumuuza nyota wake, Pierre Aubameyang msimu ujao.Awali ilikuwa inaelezwa kuwa haina mpango wa kumuuza nyota huyo msimu ujao ili kupata mkwanja mrefu wa kuutumia kwenye usajili.Timu kadhaa ambazo ilikuwa zinatajwa kuiwinda saini ya mchezaji huyo ni pamoja na Real Madrid, Barcelona na Manchester United."Auba hauzwi hakuna aliyekuja kwetu akimuhitaji nyota huyo wala nasi...
SIMBA MSIMU UJAO MCHEZAJI MMOJA KUCHEZA ZAIDI YA NAFASI MOJA, MIFUMO MPAKA MITATU
PATRICK Aussems,Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anataka kuona wachezaji wake wanacheza nafasi zaidi ya moja ili kutumia mifumo miwili au mitatu msimu ujao. Msimu uliopita, Aussems alitumia mifumo miwili zaidi, ule wa 3-5-2 hasa kipindi Shomari Kapombe akiwa fiti lakini baadaye alitumia zaidi ule mfumo wa 4-4-2.Simba inajiaanda na michuano ya kimataifa ambapo mchezo wa kwanza utakuwa kati ya...
MBEYA CITY: KAZI KUBWA ITAFANYIKA MSIMU UJAO
JUMA Mwambusi, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa kwa sasa yupo kwenye mkakati wa kukisuka upya kikosi cha Mbeya City ili kifanye maajabu msimu ujao.Mwambusi amesema kuwa kazi yake kubwa kwa sasa ni kuandaa kikosi bora kitakachofanya mambo mazuri uwanjani."Kila kitu kinakwenda sawa na msimu ujao nataka kuona timu inapata matokeo chanya kwenye mechi zetu zote tutakazocheza," amesema.Mbeya...