SIMBA QUEENS WANAPETA TU MAJUU
KIKOSI cha timu ya Simba ya Wanawake, Simba Queens bado kinaendelea na ziara yake ya wiki mbili nchini Ujerumani.Ziara hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya kujifunza bado inaendelea huku wachezaji wakitembela sehemu mbalimbali kujifunza.Miongoni mwa sehemu ambazo Simba Queens wamezitembelea ndani ya mji wa Hamburg, Ujerumani ni zile za kihistoria ili waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu utamaduni wa...
TFF: MDHAMINI MAMBO SAFI, KINACHOSUBIRIWA NI KUSAINI TU MKATABA
WILFRED Kidao, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao wa 2019/20 ameshapatikana na kinachosubiriwa ni kusainiwa kwa mkataba.Kidao ametoa taarifa hiyo wakati akijibu maswali ya wadau mbalimbali wa soka kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa shirikisho hilo, utaratibu alioamua kuufanya mara moja kila wiki.
UNITED KUMVIMBISHA MIFUKO DE GEA
DAVID de Gea anatazamiwa kusaini kandarasi mpya ya miaka mitano kuendelea kuitumikia klabu yake hiyo huku mshahara wake ukizidi kutuna.Mlinda mlango huyo hakuwa na hesabu za kuongeza mkataba mpya na iliripotiwa kwamba huenda angeibukia PSG.Kwa sasa United inaelezwa kuwa imekubali kumlipa mshahara wa pauni 375,000 sawa na sh.bilioni moja kwa wiki.Licha ya kuongezewa mshahara bado hajamfikia nyota namba moja...
PSG: ISHU YA NEYMAR KUTAKA KUSEPA ILIKUWA INAJULIKANA KITAMBO
THOMAS Tuchel, Kocha Mkuu wa Paris Saint Germain amethibitisha kwamba Neymar anataka kusepa ndani ya kikosi hicho.Tuchel amesema kuwa alifahamu ishu hiyo ya nyota huyo wa timu ya Taifa ya Brazil kutaka kusepa ndani ya kikosi hicho kabla ya michuano ya Copa America."Nilitambua wazo la nyota Neymar kutaka kusepa kabla ya michuano ya Copa America, ila linapokuja suala la...
KOCHA STARS: MDOGOMDOGO TUNATUSUA CHAN
SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania, amesema kuwa atashirikiana na bosi wake mkubwa Ettiene Ndayiragije kuifanya Stars kufanya maajabu michuano ya Chan.Stars itamenyana na Kenya, Julai 28 uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa kufuzu michuano ya Chan inayoshirikisha wachezaji wa ndani.Matola amesema kuwa ana imani na wachezaji ambao wamewateua kwa kushirikiana na kocha mkuu...
EVERTON INAVUTIWA NA EVERTON WINGA ANAYEKAMILISHA DILI LAKE KUTUA ARSENAL
ARSENAL ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na nyota wa Gremio raia wa Brazil, Everton Soares.Winga huyo mwenye miaka 23 ameongeza thamani yake baada ya kuonyesha maajabu kwenye michuano ya Copa America na amezivutia pia timu nyingi ikiwemo Everton.Hata hivyo kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho kutua Arsenal baada ya washika bunduki hao kukubaliana na Gremio kuhusu suala la...
AJIBU ALALA HOTELI YA ROONEY SAUZI
WAKATI Jeshi zima la Simba likiwa linaendelea kujifua kwenye kambi yake nchini Afrika Kusini, imebainika kuwa sehemu hiyo ambayo Simba wameweka makazi paliwahi kukaliwa na timu ya taifa ya England wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010.Simba wamekimbilia Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara sambamba na michuano...
BIGIRIMANA AANZA KUITISHA SIMBA
KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amesema kuwa katika kuthibitisha ubora wa ufungaji anaanza na AS Vita wanafuatia watani wao Simba.Staa huyo aliitoa kauli hiyo, akiwa kambini mkoani Morogoro ambako wameingia tangu Jumatatu iliyopita wakijiandaa na msimu mpya wa ligi pamoja na tamasha lao la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika Agosti 4, mwaka huu.Katika tamasha hilo, Yanga...
IGHALO SHUJAA WA NIGERIA ANAYENUKIA KUTWAA KIATU CHA UFUNGAJI BORA AFCON
ODION Ighalo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Nigeria anatazamiwa kumaliza michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri akiwa mfungaji bora.Ighalo ni shujaa wa Nigeria kwani aliipa ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo dhidi ya Tunisia ambao ulikuwa wa kumtafuta mshindi wa tatu uliochezwa Jumatano.Mpaka sasa ametupia mabao matano, akiwaacha kwa mbali washambuliaji hatari ambao ni Sadio Mane wa Senegal,...
YANGA YAZIDI KUWA YA MOTO, YAITWANGA MORO KIDS 2-0, BALINYA ATUPIA
Mabao ya Balinya na Paul Godfrey yameiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Moro Kids leo mjini Morogoro.Bao la Balinya limepatikana kwa njia ya penatiYanga imefanikiwa kupata ushindi huo ukiwa ni mchezo wa kirafiki uliomalizika muda mchache uliopita.Ushindi huo unakuwa wa pili mfululizo kwa Yanga baada ya mechi ya kwanza kushinda mabao 10-1 dhidi ya Tanzanite Academy.Kikosi...